Rosa Ree afungiwa kujiusisha na muziki miezi sita

0
376

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rosa Ree amefungiwa kujihusisha na muziki kwa miezi Sita baada ya kukutwa na makosa kupitia video ya wimbo wake wa ‘vitamin U’.

Msanii huyo amefungiwa kujihusisha na muziki kwa muda wa miezi Sita na kupigwa faini ya Millioni mbili baada ya kukutwa na makosa mawili kupitia video ya wimbo wake wa ‘vitamin U’ alioshirikiana na msanii Timmy Tdat kutokea Kenya.

Mkurugenzi wa Fedha na utawala Onesmo Kayanda ambaye kwa sasa anakaimu ofisi baada ya Katibu Mkuu wa BASATA kusafiri kikazi, amesema makosa yaliyopelekea Rosa Ree kufingiwa ni mawili ambayo kwa kila kosa ameadhibiwa kulipa millioni moja na kufungiwa muziki kwa miezi 6.

“Nikweli tumemfungia kwa miezi sita kwa makosa Mawili, Kosa la kwanza ni ishu ya maadili na kosa la Pili ni kukiuka utaratibu wa Baraza ambapo amekiuka kwenda nje ya Nchi kufanya kazi bila kupata kibali kwani taratibu zipo hivi Msanii yoyote haruhusiwi kwenda nje ya nchi kufanya kazi ya Sanaa bila kibali,

“Kwahiyo sisi kama mamlaka tumemuadhibu kwa makosa Mawili na kila kosa tumemuadhibu Millioni Moja kwahiyo jumla ni Millioni Mbili na tumemfungia kazi kwa Muda wa miezi Sita lakini mtu akishahukumiwa anaweza kupima mwenyewe kama ameonewa ama ameadhibiwa sahihi na kosa lake.

Kwahiyo tumempa siku 30 Sheria inamruhusu kwenda kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana” Alisema Onesmo Kayanda.

LEAVE A REPLY