Rosa Ree achukia kutongozwa na wanaume

0
409

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rose Ree amefunguka na kusema kuwa hakuna kitu ambacho hakipendi kama kutongozwa na mwanaume.

Rosa Ree amesema kuwa mwanaume akimtongoza hujisikia vibaya na anaweza kumchukia kutokana na kitendo hiko.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa anachohitaji ni kuwa karibu na wanaume kwa ajili ya kazi na kupiga nao stori mbalimbali lakini si kutongozana.

Amesema kuwa “Yaani mwanaume akinitongoza sipendi napenda kama tunakuwa marafiki tu wa muda mrefu kama ikitokea kupendana tutapendana mbele ya safari na si vinginevyo akinitongoza mapema naona kama ananitamani tu basi alafu animwage,”.

Rose Ree amesema kuwa kama atakuwa na ukaribu na wanaume ni sawa kutongozana mbele ya safari lakini si mapema aanze kumtpngoza.

LEAVE A REPLY