Romy Jones amuomba msamaha Baraka The Prince

0
349

Official Dj wa Diamond Platnumz, Romy Jones amemuomba msamaha mwanamuziki Baraka The Prince baada ya kumtaka kimapenzi Naj ambaye ni mpenzi wa Baraka The Prince.

Hatua ya Romy Jones kuomba msamaha imekuja baada ya Baraka The Prince kumshtumu baada ya kuona message za kimapenzi ambazo Romy Jones alikuwa anamtia Naj.

Romy Jones ametumia ukurasa wake wa Instagram kuomba msamaha huo kwa Baraka The Prince pamoja na Naj.

Ameanza kwa kuandika. NICHUKUE FURSA HII KUMUOMBA RADHI MSHKAJI,RAFIKI,NDUGU YEYE PAMOJA NA MPENZI WAKE KAMA NIMEWAKWAZA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE,NISINGEPENDA HAYA MALUMBANO YAENDELEE KWA SISI KAMA VIJANA INATUPASA TUKAE TUPANGE TUNAWEZAJE KUJIKWAMUA NA HUU UMASIKINI NA SANAA YETU KWA UJUMLA!!!!PIA NIOMBE RADHI KWA FAMILIA YANGU,NDUGU ZANGU,MARAFIKI ZANGU NA MASHABIKI ZANGU KWA UJUMLA KWA LOLOTE LILILOJITOKEZA!!! MUNGU ATUONDOLEE UADUI NA TUENDELEE KUFANYA KAZI INSHAALLAH.

Baada ya kuomba msamaha huo bado mwanamuziki Baraka The Prince hakujibu kama ameukubali msamaha huo au ameukataa.

LEAVE A REPLY