Roma Mkatoliki na Ney wana ‘BIFF’ na Madee?

0
1123

Tangu arejee kutoka safari ya Ulaya, rapa wa Tip Top Connection a.k.a Rais wa Manzese, Madee Ali ameonekana kuandamwa na ‘mikosi’.

Staa huyo aliyekwenda nchini Sweden hivi karibuni kwaajili ya kuandaa video ya ngoma yake mpya, HELA amejikuta akiwa katikati ya matatizo na maneno makali kutoka kwa wasanii wenzake na wafuatiliaji wa mambo ya burudani.

Hivi karibuni baada ya kukutwa na skendo lya kupora simu ya mama mzazi wa director wa Sweden, Makavaka baada ya kuingia kwenye mzozo wa kifedha na director huyo, Madee amejikuta tena kwenye midomo ya mastaa wenzake Ney wa Mitego na Roma Mkatoliki.

Ney wa Mitego amekuwa msanii wa kwanza kuiponda hadharani ngoma hiyo na kudai ‘ni mbaya sana’ huku ikidaiwa kuna mistari kwenye ngoma hiyo ambayo inamponda staa huyo.

Na kama haitoshi amemtaka staa wa WCB, Rayvanny amuandikie nyimbo Madee kwani ameishiwa!!

Wakati Ney akiiponda ngoma hiyo, Roma Mkatoliki nae ameibuka na kudai Madee ni staa ambaye HIP HOP imemshinda na hivyo amekimbilia kuimba.

Je, Madee ameishiwa? Au mastaa wenzake wana wivu!!