Roma awapa ushauri wasanii wa kuimba

0
40

Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Roma Mkatoliki amewashauri wasanii wa kuimba wabadilishe staili ya kuingia jukwaani wakati wanafanya show kwani wengi wao wanapenda kuingia huku wakikimbia.

Kupitia mtandao wake wa Twitter ameandika “Wasanii wa Kuimba wengi inabidi wabadilishe Style yao ya Uingiaji Jukwaani!! Wengi wanaingia kwa Kukimbia, wakifika pale mbele wanaanza kurukaruka kwa Ku- Hype!

Pia ameongeza kwa kuandika Sio kitu kibay ila isiwe sasa kila msanii. Wamuachie mmoja tu aliyeianzisha, Wasiigane igane.

Ingieni hata mnatembea tu mdogo mdogo kama hautaki Vile, mbona fresh tu!! Ukiwa mnyama na una mawe yako matatu tu ya mauaji Aaaaaah. Fans Wataamka Tu Watake Wasitake.

LEAVE A REPLY