Roma awachana wasanii wenzake

0
36

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki amewachana baadhi ya wasanii wa zamani kwa kusema wanawaangusha mashabiki zao pale wanapopewa kipaza sauti na kupanda jukwaani kufanya show.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii Roma ameandika “Nianze na neno samahani kama nitawakwaza watu lakini pia ninaweza nikawa na maana, lengo langu sio kuwadharau ama kuwavunjia heshima wasanii wa zamani.

Roma ameendelea kuandika kuwa baadhi ya wasanii wa zamanni wanatuangusha sana wanapopewa ‘mic’ na kupanda jukwaani kufanya show, mnachokitoa hakiendani na matarajio ya mashabiki”.

“Kumekuwa na malalamiko kwamba show wanapewa watu fulani lakini wengi wanaolalamika ni wasanii wa zamani kuwa hawapati nafasi lakini wanapopewa hawatumii vizuri hiyo nafasi kwanza wamesahau nyimbo zao, muda mwingi wanatumia kwenye kusema mikono juu”.

Roma ameandika malalamiko yake baada ya wasanii wa zamani kufanya show mbovu kwenye tamasha la Serengeti Festival lililofanyika mjini Dodoma.

LEAVE A REPLY