Roma aliyopitia 2018 ni kama somo kwake

0
65

Mwanamuziki wa Hip Hop, Ibrahim Musa ‘Roma’ amedai kuwa mwaka 2018 amepitia mambo makubwa na magumu lakini anamshukuru Mungu kwani yamebaki kama fundisho kichwani mwake.

Roma alisema kila mtu anajua jinsi alivyokumbana na magumu ikiwemo kutekwa ila kwake yamempa mafunzo ambayo akiingia nayo 2019 atakuwa imara tofauti na miaka mingine iliyopita.

“2019 kwangu utakuwa ni mwaka wa kazi kwani nitagusa pande zote kwa kufikisha ujumbe, hakuna atakayeweza kunifungia riziki.

Pia amesema kuwa amejipanga vema na yale yote yaliyonitokea ninamshukuru Mungu, naendelea kupambana na niwaahidi mashabiki mwaka ujao utakuwa wa tofauti,” alisema Roma.

LEAVE A REPLY