Roma akanusha Rostam kuvunjika

0
89

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini, Ibrahim Mussa ‘Roma’ amekanusha tetesi za kuvunjika kwa kundi la Rostam linaloundwa na yeye mwenyewe pamoja na msanii Stamina.

Roma amesema kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote kwakuwa kazi zao zinaendelea kama kawaida chini ya management yao.

Pia amezungumzi namna alivyomsimamiwa na Billnass katika uandishi wake wa mashairi ya wimbo huo kwa kuhofia kupeleka ujumbe mzito kwa jamii.

Tetesi za kuvunjika kwa kundi la Rostam zilishika kasi baada ya Roma kuachia wimbo wa kolabo na Billnass mwishoni mwa mwezi Januari.

Kundi hilo limeanza miaka miwili iliyopita na kufanya vizuri katika medani ya muziki wa Bongo Fleva kutokana na kazi zao.

LEAVE A REPLY