Roma ahofia maisha yake kutokana na mistari ya nyimbo zake kutokea kweli

0
179

Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Roma amefunguka na kusema kuwa kutokana na mambo mengi anayoandika katika nyimbo zake kutokea kweli muda mwingine hufikia hatua ya kuhofia maisha yake.

Roma amesema kuwa baadhi ya matukio kwenye nyimbo zake alivyoimba Rais. John Magufuli kuongoza nchini na imetokea kweli.

Pia amesema kuwa  muda mwingine mwenyewe anakaa anapitia mistari yake na anajitafakari anaona kuwa kuna kitu ndani yake.

Roma ameongeza kwa kutolea mfano nchi ya Zimbabwe ambayo imefanya mabadiliko kwenye uongozi ambapo pia wimbo wake aliuita kwa jina la Zimbabwe kwa hiyo matukio ya nyimbo zake yanashabihana.

Mwanamuziki huyo kwasasa anaunda kundi la Rostam akiwa na mwnamuziki mwenzake Stamina ambapo hadi sasa wameshaachia nyimbo mbili ‘Hivi Hama Vile na Kiba_100.

LEAVE A REPLY