Road License yafutwa, sasa kulipwa mara moja tu

0
212

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari.

Dkt. Mpango amesema kuwa uamuzi umechukuliwa ili hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na Dizeli.

Waziri Mpango amesema hayo jana wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/18 Bungeni jijini Dodoma.

Pia Waziri Mpango amesema kuwa bajeti hiyo imeshusha mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu zinazozalishwa ndani ya nchi kutoka shilingi 202 kwa lita hadi kufikia 200 kwa lita.

Ushuru wa bia zinazotengezwa kwa nafaka za ndani umepanda kutoka sh.429 hadi sh. 450 kwa lita.

Pia ushuru umepanda kwa bia zisizokuwa za kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu kutoka sh.534 hadi sh.564 kwa lita.

LEAVE A REPLY