Riyama Ally afunguka sababu ya kujikita na uuzaji wa t-shirt

0
327

Muigizaji wa Bongo Movie, Riyama Ally amesema kuwa msanii kuamua kufanya biashara haimaanishi kuwa sanaa anayofanya haimlipi bali ni kujiongezea kipato katika maisha yake.

Riyama Ally amesema hayo baada ya watu kumuambia kuwa hana jipya kwenye filamu ndiyo mana ameamua kuanzisha biashara ya t-shirt jambo ambalo amelipinga vikali.

Muigizaji huyo amesema kuwa msanii hapaswi kutegemea sanaa pekee kama njia ya kujiingizia kipato na ndio sababu ya yeye kuamua kuanzisha biashara hiyo.

Riyama amedai kushangazwa na watu hao ambao wamekuwa wakimdhihaki baada ya kuamua kujikita katika biasha za t-shirt ambazo amezipa jina la ‘Sonyo’.

Ikumbukwe kuwa mbali na mugizaji huyo kujikita kwenye biashara zake binafsi pia ni balozi wa kampuni ya DSTV.

LEAVE A REPLY