Ripoti ya ‘Maafa ya Kagera’ kukabidhiwa Serikalini

0
171

Serikali inatarajia kupokea ripoti ya Kamati ya Maafa ya Kagera ambayo itaonyesha athari na mchanganuo wa jitihada za Serikali, wananchi na wadau wengine na mahitaji yaliyopo kwenye mkoa wa Kagera.

Mkoa wa Kagera ulikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17 na majeruhi zaidi ya 200.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, amesema kuwa serikali imejipanga kuikagua taarifa hiyo na kujiridhisha kabla ya kuendelea na zoezi la umaliziaji wa ukarabati wa miundombinu ya maeneo yaliyoharibiwa.

Waziri Mhagama amesema kuwa kamati yake itahakikisha fedha zilizopatikana zinatumika kurekebisha miundombinu ya Serikali.

‘Huduma muhimu za kijamii kama vile shule, hospitali na miundombinu ya barabara ndio kipaumbele chetu hivyo tutahakikisha tunafanya haraka iwezekanavyo view kwenye hali nzuri ya kutoa huduma’.

LEAVE A REPLY