RIP: Prodyuza wa Backstreet Boys na *NSYNC, Lou Pearlman amefariki

0
101
Lou Pearlman (Photo by Steve Granitz/WireImage for The Recording Academy (View ONLY)) *** Local Caption ***

Prodyuza wa zamani wa makundi yaliyowahi kutamba kwenye muziki wa Marekani na duniani ya *NSYNC na the Backstreet Boys, Lou Pearlman amefariki dunia.

Pearlman ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwenye kutamba kwa makundi hayo kwenye miaka ya 90 amefariki gerezani akiwa na miaka 62.

Pearlman alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 25 kwenye gereza la Federal Correctional Institution lililopo Texas.

Alikutwa na hatia na kuhukumiwa mwaka 2008 kwa udanganyifu na ulaghai wa zaidi ya $300m.

Hata hivyo sababu za kifo chake hazijatangazwa.

Pearlman atakumbukwa kwa uwezo wake mkubwa pale aliposaidia kuundwa kwa makundi ya Backstreet Boys ambalo alilitengenezea hit za ‘I Want It That Way’ na ‘Quit Playing Games (with my Heart)’ kabla ya kuwatengenezea ‘Bye Bye Bye’ kundi la *NSYNC.

Makundi hayo ndiyo yaliyokuja kuwatoa mastaa wa Marekani kama Boy Nick Carter kutoka kundi la Backstreet Boys na mkali wa zamani wa kundi la  *NSYNC Justin Timberlake.

Mastaa kadhaa akiwemo Timberlake wameonyesha kuguswa na msiba huo na aliandika kupitia Twitter ‘I hope Pearlman had found some peace.’

Pia wakili wa zamani wa Pearlman Mark NeJame nae aliandika ‘His passing has touched a lot of people’

‘He literally revolutionized the world of pop music and [he was] a creative genius in that regard — but [he] had a horrible dark side that eventually overshadowed his talents’

Wakati wa kilele cha ubora wa Pearlman, kundi la Backstreet Boys lilikuwa moja miongoni mwa makundi machache lililoweza kuuza zaidi ya milioni 130.

Kisha alipoliibua kundi la *NSYNC alilisaidia kuuza zaidi ya nakala milioni 55.

Makundi hayo kwa sasa ni kama hayapo huku wasanii wake wakijikita zaidi kwenye kazi binafsi.

 

LEAVE A REPLY