Rihanna apata shavu kwenye tamthiliya ‘Bates Motel’

0
173
Staa wa Pop, Rihanna amefanikiwa kupata fursa nyingine ya kuonyesha uwez wake wa uigiaji baada ya kuchaguliwa kuigiza nafasi muhimu kwenye tamthiliya ya ‘Bates Motel’.
Uteuzi huo wa Rihanna uliwekwa wazi Ijumaa kwenye kongamano la
Comic-Con International lililofanyika kwenye jimbo la San Diego nchini Marekani ambapo waandaaji na waigizaji walikuwa na kongamano la pamoja.
Waandaaji wa tamthiliya hiyo walipost video ya staa huyo kupitia mtandao wa twitter akitangaza kuhusu uteuzi huo.
Licha ya kufahamika kwa ukali wa ngoma zake kama vile ‘Work’, ‘Umbrella’, na ‘What’s My Name’, Rihanna ameshashiriki kwenye filamu kadhaa ‘Battleship’ na ‘This is the End’.
Ushiriki wake kwenye msimu wa tano na wa mwisho wa tamthiliya ya ‘Bates Motel’ utampa nafasi ya kucheza pamoja na mastaa wengine kama vile Vera Farmiga, Freddie Highmore, Max Thieriot, Olivia Cooke na Nestor Carbonell.

LEAVE A REPLY