Rihanna aingiza sokoni bidhaa zake

0
154
Rihana

Mwanamuziki wa Marekani, Rihanna aingia rasmi kwenye biashara ya vipodozi vya ngozi, ameisajili kibiashara kampuni iitwayo “Fenty Skin” March 25.

Kwa miaka miwili sasa kampuni yake ya vipodozi na mavazi ‘Fenty Beauty’ imekuwa ikifanya vizuri kwa kuingiza sokoni bidhaa kama Make Ups, Miwani, viatu na mavazi mbali mbali.

Sasa Riri yupo tayari kukuletea mafuta ya ngozi na bidhaa nyingine kwa ajili ya ngozi yako kutokana na bidhaa zake hizo mpya.

Kwa mujibu wa Bernard Arnault, mwenyekiti na Mkurugenzi wa kampuni hiyo aliweka wazi kuwa mauzo ya bidhaa za Fenty Beauty yalifikia kiasi cha Tsh. Trilioni 1.3 hadi mwaka 2018.

Mwanamuziki huyo amejiungiza kwenye biashara hiyo ili kujiingizia kipato kingine nje ya muziki na anafanya vizuri sana kwenye biashara hiyo.

LEAVE A REPLY