Ridhiwani Kikwete amempongeza Makonda kwa kupambana na dawa za kulevya

0
361

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga vita dawa za kulevya.

Ridhwani ameishauri serikali kuifikisha mwisho vita hiyo ili kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa.

Mbunge huyo ametolea mfano uwezo wa msanii wa Bongo Fleva, Langa ambaye kwa sasa ni marehemu ikidaiwa kuwa alipoteza maisha kutokana na dawa hizo, pamoja na shida alizokuwa akizipata msanii Ray C.

Pia ameitaka mamlaka mpya wa dawa za kulevya kuwachunguza watu 97 ambao majina yake yamekabidhiwa hivi karibuni na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na yeyote atakayethibitika kuhusika, achukuliwe hatua, huku akionesha imani kubwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Rogers William Sianga.

 

LEAVE A REPLY