Real Madrid imekuwa timu ya kwanza kufikisha goli 6,000 ndani ya La Liga

0
179

Klabu ya Real Madrid imekuwa timu ya kwanza kufikisha magoli 6,000 kwenye ligi ya La Liga baada ya jana kushinda 5-3 dhidi ya Real Betis.

Katika mchezo huo bao la pili la Marco Asensio ambalo alifunga dakika ya 59 ndio liliifanya Real Madrid kutimiza mabao 6,000 ya kufunga kwenye ligi hiyo na kuwa timu ya kwanza kufikia idadi hiyo kubwa ya mabao.

Baada ya bao hilo la pili la Asensio lilikuja muda mfupi tu baada ya beki Sergio Ramos kufunga bao la 5,999 ambapo baadae pia Madrid waliongeza mabao mawili kupitia kwa Cristiano Ronaldo na Karim Benzema na kufanya wafikishe jumla ya mabao 6,002.

Baada ya ushindi huo wa jana Madrid imefikisha alama 45 na kuendelea kusalia nafasi ya nne kwenye msimamo wa La Liga ikiwa nyuma ya Valencia, Atletico Madrid na vinara Barcelona wenye alama 62 kileleni.

LEAVE A REPLY