RC Makonda awataka wananchini kuchukua tahadhari kuhusu mvua

0
100

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa tahadhari kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuchukua tahadhari kwa mvua zinazoendelea kunyesha.

Makonda amewataka wananchi kukaa maeneo salama kwa ajili ya usalama wao na mali zao kwa ujumla.

Makonda amesema kuwa utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa leo Aprili 16, 2018 mvua hizo zitakua kubwa zaidi hivyo wananchi hawana budi kuchukua tahadhari mapema zaidi.

Pia Makonda amewatahadharisha madereva wa magari kuwa makini na barabara kwani miundombinu imeharibuka kutokana na mvua hiyo.

Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha vifo vya watu saba baada ya kusombwa na maji.

LEAVE A REPLY