RC Makalla akanusha kuandika barua ya kumuomba radhi Rais Magufuli

0
166

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amekanusha taarifa kuwa, anakusudia kuandika barua ya kumuomba radhi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. John Magufuli kwa kushindwa katika uchaguzi Kata ya Ibighi.

Makalla amenusha taarifa hizo zilizosambaa mtandaoni tofauti na alichokisema yeye katika mkutano wa (UWT) mkoa uliofanyika jana ambapo alikuwa msimamizi Mkuu wa uchaguzi.

“Nilichowaasa wajumbe wa mkutano na wanaCCM, watafakari kwanini Chama cha Mapinduzi kimeshindwa katika uchaguzi Kata ya Ibighi na zaidi nilisema Chama mkoa wa Mbeya kifanye tathmini kwanini mikoa mingine wamefanikiwa kushinda na CCM Mkoa wa Mbeya kushindwa Kata ya Ibighi,  nikashauri Chama kifanye tathmini ngazi ya kata , Wilaya na Mkoa kujua tatizo ni nini,”.

Alisema, ni kwa ajili hiyo akashauri Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya wamuombe radhi Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Magufuli kwa kupoteza Kata hiyo.

Amesema kuwa “Mimi sikuhaidi kuandika barua ya kuomba radhi na habari zichukuliwe ni za uongo na uzushi,”.

LEAVE A REPLY