Rayvanny na Hamisa waachiwa kwa dhamana

0
69

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny pamoja na mwanamitindo, Hamisa Mobeto wameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Japhet Kibona, amesema ni kweli  wasanii Hamisa Mobetto na Rayvanny walikuwa wanashikiliwa na polisi kituo cha Osterbay lakini wameachiwa kwa dhamana na uchunguzi bado unaendelea kufanyika.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Japhet Kibona ameeleza kuwa “Ni kweli walikamatwa jana, hii ni kesi ya polisi na hupaswi kueleza walichokizungumza ni nini ila kilichopo ni kusambaza picha kwenye mtandao bila ridhaa ya mmoja wapo mwenye hizo picha, Hamisa na Rayvanny walidhaminiwa wote”.

“Tunaendelea na uchunguzi kwa kilichofanyika na uchunguzi wetu na upelelezi ndio utakaoridhia, pia kuna Mwanasheria ambaye atapitia kama kilichofanyika ni kosa la kijinai au la” ameongeza

Rayvanny anadaiwa kuvujisha video mitandaoni akiwa ana-kiss na mtoto wa staa wa filamu Kajala Masanja ambaye ni mwanafunzi Paulah Kajala, na Hamisa Mobetto anadaiwa ndiyo alimpeleka mtoto huyo kwa Rayvanny.

LEAVE A REPLY