Rayvanny kuondoka WCB kwa amani

0
66

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny aliyepo chini ya label ya WCB amesema kuwa atahakikisha anatoka kwenye label hiyo kwa amani kama atataka kutoka.

Rayvanny alisema jambo hilo linawezekana, na wanaosema hayo wanaongea kwa kuwa yeye ni msanii anayefanya vizuri WCB.

Rayvanny alisema kama ukifika wakati wa yeye kuondoka WCB basi atahakikisha anaondoka kwa amani bila migogoro yoyote.

Katika mambo mengine aliyosema Rayvanny ni kwamba yeye hanywi pombe, havuti sigara wala bangi hata hivyo alikataa kutaja starehe anayoipenda.

Amedai yeye ni mtu anayemtegemea na kumwamini Mungu na kwamba mama yake ni mlokole wa dhehebu la Baptist huko mkoani Mbeya ambapo pia amedai yeye alikuwa akiimba kwaya kanisani.

Anasema hajawahi kwenda kwa mganga na haamini katika kutegemea nguvu za giza na katika kuthibitisha ucha Mungu Rayvanny amesema watu wasijeshangaa siku akiacha Bongo Fleva  na kuhamia kwenye muziki wa Injili.

LEAVE A REPLY