Rayvanny awaangukia Basata kuhusu wimbo wa Mwanza

0
136

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny ameibuka na kuwaomba tena BASATA wampe ruhusa ya kuperfom wimbo wa Mwanza stejini.

Wiki chache ziliopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liliufungia rasmi wimbo wa ‘Mwanza’ wa Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kwa kuimba matusi.

Rayvanny alisema angetamani sana kwa mara ya kwanza apafomu Wimbo wa Mwanza katika jukwaa la Wasafi Festival lakini anashindwa kutokana na adhabu ya Basata ya kuufungia wimbo huo ambao yeye anakiri kuwa hakuutunga kwa nia ya kupotosha watu bali kuburudisha.

WCB wanategemea kupigwa bonge la shoo kwenye tamasha Lao la Wasafi Festival linalotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumamosi hii tarehe 24 mkoani Mtwara.

LEAVE A REPLY