Rayvanny amuomba msamaha Kajala Masanja

0
83

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ametumia ukurasa wake wa Instagram kumuomba msamaha Kajala Masanja baada ya kusambaza video za ngono akiwa na Paula mtoto wa Kajala.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameanza kwa kuandika Duniani wakati mwingine kuna vitu tunavifanya ambavyo pengine kwa macho yetu ya ujana tunaona ni sahihi lakini tunasahau upande mwingine wa pili ambao ni wazazi wanaoumia kwa namna moja au nyingine.

Pia ameandika Nichukue nafasi hii kumuomba radhi dada angu Kajala na kuwaomba radhi wazazi na yoyote ambaye nilimkwaza kwa kupost video ambayo inawezekana imetafsiriwa vibaya.

Ameongeza kwa kuandika Kwasababu sisi ni binadamu na kamwe hatuwezi kukamilika, alimalizia kwa kuandika mwanamuziki huyo kutoka lebo ya WCB.

LEAVE A REPLY