Rayvanny ampa ushauri mzito bosi wake Diamond

0
357

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amemshauri bosi wake Diamond Platnumz kuhusu changamto anazokutana nazo kwenye kazi yake ya muziki.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa hakuna anayefanikiwa akakosa maadui na ndicho kinachotokea kwa Diamond sasa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny ameandika;

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameanza kwa kuandika “Kuna Vitu Pengine Unaweza Ukawa Unapatia Au Vingine Unakosea Sitaki Kuongelea Hilo Sababu we nawe Ni Binadamu. ILA KWENYE KUSEMA UKWELI NITASEMA!!!! Si kwa Sababu wewe Ni boss Wangu Hapana!!! Ila Mara Nyingi Thamani Ya mtu Na Umuhimu Wa Mtu wengi Wanaujua Akishaondoka…. MZIKI NI KAZI NA NI AJIRA Namaanisha Kuna Familia Nyingi Zinaishi kupitia Huu huu mziki”.

Pia ameandika “DIAMOND KATIKA WASANII WOOOTE Umekua chachu Ya Kuongeza Thamani Ya Muziki Nakupitia wewe naamini Wengi Wanafanikiwa…. KUJITOA KWAKO, KUAMINI KATIKA UMOJA NA PIA KUTHUBUTU Ndiko kunafanya Unafanikiwa…. USHAAMBIWA HUJUI KUIMBA ila ukaimba ukafanikiwa… USHAAMBIWA UNAVIMBA UNAIGIZA MAISHA Lakini sasa Unayaishi hayo Maisha… Hakuna Anaefanikiwa Akakosa maadui ndivyo Dunia Ilivyo”.

Ameongeza kwa kuandika “MIMI ULINISAIDIA ULIJUA SHIDA ZANGU Naamini Mungu Alikutumia wewe Ukawe Mkombozi Wangu ……. KWAIO KUMBUKA ( ILI MBEGU IOTE LAZIMA IOZE ) SINA MUDA KUMSEMA MTU ILA NAKUPA MOYO FANYA KAZI SIMBA……. kama Wewe Unaamini Katika Upendo Na sio Chuki, Vita Na Matusi JUS COMMENT ( LOVE )

LEAVE A REPLY