Rayvanny amkimbiza Harmonize Youtube

0
167

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amemfikia idadi ya mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Harmonize ambaye ni mmiliki wa Konde Music Worldwide.

Rayvanny amefikisha jumla ya subscribers Milioni 1.64 akiifikia idadi ya Harmonize ambayo ni hiyohiyo Milioni 1.64.

Tofauti iliyopo kwa sasa kati ya Rayvanny na Harmonize kwenye mtandao wa YouTube ni jumla ya watazamaji kwenye channel zao.

Harmonize ametazamwa na watu zaidi ya Milioni 373.9 huku Rayvanny akitazamwa na watu zaidi ya Milioni 296.1 kwenye youtube yake.

Diamond ndiye anayeongoza kwa kuwa na wafuasi Milioni 3.4 huku akiwa ametazamwa na watu zaidi ya Milioni 954.6.

LEAVE A REPLY