Rayvanny alivyofanya kazi na Cuppy wa Nigeria

0
22

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amevuka boda baada ya kufanya kazi na mwanamuziki Cuppy kutoka nchini Nigeria.

Katika singo hiyo mpya inayokwenda kwa jina la Jollof On The Jet iliyoachiwa hewani kwa mara ya kwanza juzi Jumamosi, yupo mwanamuziki mwingine kutoka Nigeria, Rema ambaye naye ameonesha makali yake.

Jollof On The Jet ni ngoma yenye mirindimo ya Afro-Pop, ambayo kwa pamoja; wasanii Cuppy, Rayvanny na Rema wameutendea haki.

“Kiukweli mseto wangu na Rayvanny na Rema ni wa kipekee. Tumerekodi tukiwa mbalimbali, haikuwa rahisi kuwa pamoja studio. Kila mmoja alirekodi kivyake kisha kazi ya kuchanganya sauti ikafanywa studio. Naamini hii ni kazi bora kabisa.”

Makali ya Cuppy yalianza kudhihirika tangu mwaka 2014, alipochaguliwa kuwa DJ bora wa mwaka katika Tuzo za Muziki za MTV (MTV Africa Music Awards).

Ngoma nyingne za Cuppy zinavyotingisha ni Green Light akiwa na Tekno na Gelato akiwa na Zlatan.

LEAVE A REPLY