Ray na JB kuzichapa ulingoni sikukuu ya Pasaka

0
91

Waigizaji wa Bongo Movie, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Stephen ‘JB’ wanatarajia kupambana katika pambano la ndoni litakalofanyika mkoani Morogoro.

Wawili hao watapanda ulingoni kwenye sherehe ya sikukuu ya Pasaka ambapo kila mmoja amejitamba kumpiga mwenzake.

JB akijifua kwa ajili ya pambano hilo.
JB akijifua kwa ajili ya pambano hilo.

Kwa upande wa Ray amesema kuwa atahakikisha anammaliza mpinzani wake mapema kabla ya raundi 12 kumalizika kwani amejipanga vizuri na anatarajia kummaliza na kumpiga KO.

Naye JB amesema kuwa kwa upande wake amejipanga vilivyo na amepata mazoezi ya kutosha kutoka kwa kocha wake hivyo anasubilia siku ifike ili haweze kutoa dozi kwa msanii mwezake huyo.

LEAVE A REPLY