Ray C awataka watanzania kumsaidia Rose Mhando

0
165

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amewataka watanzania wote kuungana na kumsaidia msanii wa nyimbo za injili Rose Muhando.

Ray C amesema hayo baada ya hivi karibuni kusambaa kwa kipande cha video kikimuonesha Rose Muhando akiwa katika maombezi huku hali yake ikionekana siyo nzuri kabisa.

Ray C ameweka wazi kuwa mpaka hivi sasa Rose Muhando yupo tu nchini Kenya ambapo makazi yake yapo lakini hana msaada wowote hivyo ameitaka serikali na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kumsaidia Rose Muhando.

Ray C amefunguka hayo kupitia akaunti yake ya Instagram kwa kuwaomba watanzania kumsaidi mwanamuziki huyo maarufu wa mioandoko ya injili.

LEAVE A REPLY