Ray awachana wanaosema ‘Kanumba kafa na Bongo Movie’

0
637

Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Vincent Kigosi (Ray) kupitia ukurasa wa Instagram amewachana baadhi watanzania kwa kuwaita wanafiki baada ya kusema  Kanumba amekufa na Bongo Movie.

Ray Kigosi amesema kuwa unafiki huo wa baadhi ya watu ulimfanya mpaka marehemu Kanumba kuvunjwa moyo katika kazi zake za sanaa.

Kupitia ukurasa wake huo Ray ameandika

“Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, mara anatumia nguvu za giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza. Kanumba alipoenda ‘Big Brother’ alipondwa sana na kuitwa bogus kwa madai hajui kiingereza, ni watanzania hawa hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. Lakini leo wanamsifia hakuna kama Kanumba. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. Ila alisema maneno machache kuwa mtanikumbuka kama si leo basi ni kesho na alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba”.

Pia aliandika “Je, Kanumba kaondoka na bongo movie yake ya Freemanson? Kama wengine mnavyodhani Industry ni mtu sio system”.

Ray ameamua kuandika maneno hayo kutokana na soko la Bongo movie kushuka kwasasa huku baadhi ya watu wakisema kuwa Kanumba kafa na Bongo Movie wakati kipindi alipokuwa hai walikuwa wanamponda sana na hao hao ndiyo wanaomkumbuka kwasasa.

LEAVE A REPLY