Ray asema angekuwa waziri wa Sanaa angewachuja wasanii

0
288

Muigizaji wa Bongo Movie, Vicent Kigosi ‘Ray’, amesema kuwa kama angeteuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, angeanzisha mpango maalumu wa kuwachuja wasanii.

Ray amedai kuwa kila mtu anataka kuwa msanii, hakuna mgawanyiko wa kazi katika sanaa ya Bongo kutokana na kuvamiwa na watu wasiojua sanaa ni nini.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kuwa msanii akicheza filamu moja basi kesho ameshakuwa staa na anavaa kofia zote kama vile utayarishaji, uongozaji na uigizaji.

Pia Ray amemshauri Dk. Harrison Mwakyembe kuwa aliangazie soko la filamu Bongo kwani sinema za kizungu zinauzwa shilingi 700 na filamu za hapa Bongo ni shilingi 2500.

Ray amedai kuwa filamu hizo zinauzwa gharama hiyo kwa kuwa zinauzwa bila ya kulipiwa kodi.

LEAVE A REPLY