Ray akanusha kuanzisha mahusiano mapya

0
164

Muigizaji wa Bongo Movie, Ray Kigosi amekanusha kutoka kimapenzi na muigizaji mwenzake wa Bongo movie Sarafina baada ya kuachana na mzazi mwenzake, Chuchu Hansy.

Ray amefunguka hayo baada ya kuenea kwa taarifa kuwa msanii huyo kwasasa anatoka na mwanadada Sarafina ambaye nae pia ni muigizaji wa Bongo Movie.

Muigizaji huyo amesema kwamba hawezi kuzuia watu kuongea, lakini ameamua kuachana nao huku akiangalia zaidi mustakabali wa maisha yake.

Ray amesema kuwa yeye taarifa hizo anazisikia ila hawezi kumzuia mtu kuongea ila ukweli anaujua yeye mwenyewe kwani walishamzushia mambo mengi tu ila mambo bado yanaenda.

Kwa upande wa Chuchu Hans amesema kwamba kwa sasa hana muda wa kumfuatilia Ray kwani kama ameshaamua kufanya hivyo hawezi mzuia, na ameshazoea kuumizwa kwenye mahusiano.

Chuchu Hansy amesema kuwa “unajua kuna wakati mtu unaishiwa hata maneno ya kusema, halafu kingine sina muda tena wa kumfuatilia mtu na kama kaamua hivyo sawa ni kwa faida yake maana wengine tushazoea kuumizwa siku zote”.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa wawili hao hawapo pamoja tena, huku Ray akitajwa kuwa kwenye mahusiano mapya na muigizaji wa bongo movie, Sarafina.

LEAVE A REPLY