Rasmi: Afande Sele ajiunga CCM

0
224

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele leo amejiunga rasmi na Chama Cha Mapunduzi (CCM).

Afande Sele amepokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha sigara kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro mapema leo.

Baada ya kupokelewa Afande Sele amesema kuwa anashukuru kupokelewa ndani ya Chama hicho kwani anajua watampa ushirikiano.

Mwanamuziki huyo aliwahi kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo kabla ya kujivua uanachama ambapo aligombea ubunge katika jimbo la Morogoro Mjini kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2005.

Afande Sele ameungana na msanii mwenzake, Kala Pina aliyejiunga na CCM akitokea chama cha ACT – Wazalendo.

LEAVE A REPLY