Rashford, Defoe waitwa kikosi cha Uingereza

0
159

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ameitwa kwenye kikosi cha kocha wa England , Gareth Southgate.

Rashford mwenye umri wa miaka 19 hapo awali alitarajiwa kushirikishwa katika upande wa vijana mwenye chini ya umri wa miaka 21 watapokuwa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Denmark wikendi ijayo.

Washambuliaji wa England Harry Kane na Wayne Rooney wote wametolewa kutokana na majeraha, huko Rashford akitarajiwa kuchukua nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine, kocha Southgate amemwita kikosini mshambuliaji mkongwe wa Sunderland, Jermaine Defoe ambaye kwa kipindi cha miezi zaidi ya sita amekuwa akionyesha kiwango cha hali ya juu.

England itakabiliana na Ujerumani katika mechi ya kirafiki kabla ya mchuano wa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania huko Wembley tarehe 26 mwezi Machi .

Rashford alifunga goli katika mechi yake ya kwanza na England walipopata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Australia mwezi Mei mwaka Jana na wamejizolea vikombe sita vikuu.

LEAVE A REPLY