Rapa Molemo ‘Jub Jub’ Maarohanye aachiwa kwa msamaha

0
211

Rapa mtata wa Afrika Kusini Molemo ‘Jub Jub’ Maarohanye, ambaye aliua watoto wanne wakati wa onyesho la mashindano ya magari ya kuvuta mizigo mwaka 2010 ameachiwa kwa msamaha kutokana na kuonyesha tabia njema gerezani.

Rapa huyo na mwenzake Themba Tshabalala walihukumiwa vifungo vya miaka 20 jela kwa mauaji mnamo mwaka 2012 lakini hukumu yao ilibadilishwa na kuwa mauaji ya bila kukusudia na adhabu yao kupunguzwa hadi miaka 10.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na mtandao wa eNCA zinadai kuwa washtakiwa tayari wameshatumikia wametumia vifungo vyao kwa miaka minne na mwezi mmoja kila mmoja.

Kwenye tukio la ajali la mwaka 2010 wanafunzi wanne walifariki dunia papo hapo: Prince Mohube, Mlungisi Cwayi, Andile Mthombeni na Phomello Masemola huku Frank Mlambo na Fumani Mushwana wakipata ulemavu wa kudumu wa ubongo.

LEAVE A REPLY