Ranieri: Nataka Conte ashinde ligi kuu

0
163

Kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri amesema anataka kocha wa Chelsea, Antonio Conte ashinde kombe la Ligi kuu nchini Uingereza.

Ranieri mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Leicester kushinda taji la ligi kuu msimu uliopita.

Leicester kwasasa inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi kuu nchni Uingereza ikiwa na alama 34.

Kocha huyo amesema kuwa akiwa kama kocha wa zamani wa Chelsea na mshabiki wa Italia anatamani Conte ashinde taji la ligi ya Uingereza.

Ranieri ana mkataba Leicester hadi 2020 lakini anakubali kwamba nafasi yake katika klabu hiyo haiko salama, licha ya kufikia ufanisi wa kushangaza msimu uliopita.

Pia amesema kuwa “Ninahisi vyema hapa, ingawa katika kandanda mnakuwa juu kwenye nyota leo na kesho yake mnajipata chini sakafuni, kwa hivyo usiwahi kudhania umefika.”

 

LEAVE A REPLY