Rais wa Zimbabwe afanya ziara Afrika Kusini

0
53

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amefanya ziara ya kwanza nje ya Taifa tangu aapishwe mwezi uliopita kwa kutembelea Afrika Kusini.

Msemaji wa Rais, Bongani Ngqulunga amesema Mnangagwa jana Desemba 21,2017 alimtembelea Rais Jacob Zuma mjini Pretoria.

Viongozi hao wawili watazungumzia masuala muhimu ya maendeleo ya kikanda, Bara la Afrika na kimataifa.

Kwa mujibu wa ubalozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini, Rais Mnangagwa anatarajiwa kutumia fursa hiyo kuvutia uwekezaji kutoka nchi hiyo jirani.

LEAVE A REPLY