Rais wa Nigeria azindua rasmi Treni za mwendokasi

0
191

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ameazindua rasmi usafiri wa treni za kisasa zilizo na uwezo wa kuendeshwa kwa mwendo wa kasi nchini humo.

Mradi huo wa kwanza kwa Nigeria umeigharimu nchi hiyo dolla million $850 .

Reli hizo za kisasa kwa mfumo uitwao standard gauge(SGR) zilijengwa na kampuni kutoka Uchina.

Reli hizo ambazo ni mbili kwa moja yaani moja ni ya kwenda na nyengiine ya kurudi, zinaunganisha miji ya Abuja na Kaduna ambapo treni zitaweza kusafiri kwa mwendo wa kasi ya kilomita 120 hadi 150 kwa saa.

Wakati wa ufunguzi huo rais Buhari mwenyewe amesafiri kwa treni hiyo hivyo kuuanzishwa mfumo huo wa usafiri wa reli kwa umma.

Nauli kutoka mji huo mkuu wa Nigeria Abuja hadi mji wa Kaduna ulioko jimbo la kazkazini mwa nchi hiyo ni dolla $1:50 pekee.

LEAVE A REPLY