Rais wa Misri kuwasili nchini kwa ziara ya siku mbili

0
128

Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi anatarajia kuwasili siku ya Jumatatu ya wiki ijayo kwaajili ya ziara ya siku mbili ambapo ataongozana na ujumbe wake na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda mbele ya waandishi wa habari kuhusu ugeni huo hapa nchini.

Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam ikiwemo wenye Hotel, Magari na Migahawa kuchangamkia fursa ya ugeni huo katika kufanya biashara ili kujipatia kipato na kukuza Biashara zao.

Pia Makonda amewataka wakazi wa Dar es salaam kuonyesha ukarimu tangu Rais atakapowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere hadi hapo atakaporejea nchini Misri siku ya Jumanne.

Ugeni huu ni matunda ya uwezo wa Rais Magufuli katika kujenga mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali ulimwenguni.

LEAVE A REPLY