Rais wa Gambia Yahya Jammeh aachia madaraka kwa amani

0
278

Rais wa Gambia, Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka ya urais kwa amani kufuatia kushindwa uchaguzi mkuu wa nchi kwa kupata 36.7% ya kura zote huku mpinzani wake Adama Barrow akijikusanyia 45.5% ya kura zote.

 Rais Jammeh ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 22 aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari vya magharibi akidai kuwa ataingoza nchi hiyo hata kwa miaka bilioni endapo Mungu angependa.

Kushindwa huko kwa rais huyo kumekuja kati hali ya kushangaza kufuatia kauli ya rais huyo kuwa alitarajia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo.

Rais Jameh aliingia madarakani tangu mwaka 1994, kufuatia mapinduzi ya kijeshi hata hivyo aliendelea kuungwa mkono na wananchi wan chi hiyo kwenye chaguzi za kidemokrasia zilizofuatia.

Mwezi uliopita rais Jammeh alitanga kuiondoa nchi ya Gambia kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC ikiwa ni hatua ya kupinga mwenendo wa mahakama hiyo.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, Bwana Barrow amepata kura 263,515 na rais Jammeh amepata kura 212,099.

LEAVE A REPLY