Rais wa FIFA kuwasili nchini Februari 22

0
168

Rais wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), Gianni Infantino anatarajiwa kuwasili nchini Februari 22 kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA

Baada ya kuwa hapa nchini, Infantino ataonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.

Hayo yamethibitishwa na Waziri Mwakyembe kuwa Rais wa FIFA anatarajia kuwasili nchini usiku wa saa nane kuamkia Februari, 22  mwaka huu 2018 ambayo ndiyo siku ya mkutano na saa tatu asubuhi yake ataelekea Ikulu kukutana na viongozi wakuu wa nchi.

Kwa upande Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wilfred Kidao akisema mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili Maendeleo ya Soka la Wanawake, Maendeleo ya Soka la Vijana, Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.

Infantino anatarajiwa kuondoka nchini mara baada ya kumaliza mkutano wake na kushiriki chakula cha jioni.

LEAVE A REPLY