Rais wa FIFA awasili nchini

0
137

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amewasili Dar es Salaam kwa ajili ya kongamano maalumu la kutathmini maendeleo ya mpira wa miguu.

Baada ya kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, Infantino amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Baada ya Infantino kuingia kuchaguliwa Rais wa FIFA mwaka 2016 alipendekeza kufanya makongamano yatakayofahamika kama The Executive Football Summits.

Makongamano haya ni moja ya jitihada za msingi za Infantino kuleta mabadiliko ndani ya FIFA kwa kutoa jukwaa la kubadilishana mawazo na uzoefu sambamba na kuongeza ushirikishwaji wa wanachama wote wa FIFA katika maamuzi ya kimkakati ya shirikisho hilo.

LEAVE A REPLY