Rais Trump ashtakiwa Mahakamani kwa ubakaji

0
107

Idadi ya wanawake wanaomshtaki Rais wa Marekani Donald Trump mahakamani kwa madai ya kuwa na uhusiano nao kimapenzi inaendelea kuongezeka ambapo sasa wamefika wanawake watatu.

Mtaalamu wa kujenga mwili na Mwanamitindo Karen McDougal alifungua kesi jana March 20, 2018 kwenye Mahakama ya Juu jijini Los Angeles akiwa anahitaji haki ya kuzungumza hadharani kuhusu uhusiano wake na Rais Trump.

Huyu ni mwanamke wa pili, baada ya Staa wa sinema za ponografia Stormy Daniels pia kufungua mashtaka dhidi ya Rais Trump mwanzoni mwa mwezi March, 2018.

Jana hiyo hiyo pia, Mahakama ya Juu ya New York ilieleza kuwa mashtaka mengine dhidi ya Rais Trump yamefunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kipindi cha television Marekani cha The Apprentice, Summer Zervos akidai kuwa alibakwa na Rais huyo.

LEAVE A REPLY