Rais Salva Kiir amuondoa madarakani makamu wa rais Riek Machar

0
188

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir ametengua uteuzi wa makamu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar kufuatia mapigano na uhasama baina yao ambao umezua mauaji ya watu zaidi ya 1,000.

Badala yake rais Kiir amemteua Jenerali Taban Deng kushika wadhifa huo.

Hatua hiyo imefuatia kukosekana kwa makamu huyo wa rais kwenye vikao vya usuluhishi ambapo rais Kiir alimpa hadi Jumamosi iliyopita kuweza kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano.

Baada ya Machar kukosekana Jumamosi, wanachama wa chama chake walifanya kikao na kumteua Jenerali Deng kuchukua nafasi yake.

Hata hivyo msemaji wa Machar, Nyarji Roman amesema hatua hiyo ni njama ya kumpindua bosi wake ambaye inadaiwa alishamfukuza kazi Jenerali Deng.

Kabla ya kuteuliwa kuwa makamu wa rais, Jenerali Deng ndiye aliyekuwa mwakilishi wa Riek Machar kwenye mikutano ya upatanishi hivyo mageuzi hayo huenda yakazidi kutatiza juhudi za kupatikana kwa amani ya kudumu nchini humo.

Sudani Kusini ilipata uhuru wake mwaka 2001 kutoka nchi ya Sudan lakini ikaingia kwenye machafuko miaka miwili baadae baada ya rais Salva Kiir kumtuhumu mpinzani wake Riek Machar kupanga njama za kumpindua.

LEAVE A REPLY