Rais Rungu aamuru vikosi vya kijeshi kukabiliana na kipindupindu nchini Zambia

0
97

Rais wa Zambia, Edgar Lungu ameamuru vikosi vya kijeshi na polisi wasaidiane na maafisa wa matibabu katika kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu ambacho tayari kimesababisha vifo vya watu 41 katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Msemaji wa rais Amos Chanda, ameeleza kuwa maradhi hayo yalikuwa yameathiri zadi maeneo yaliyo na wakaazi wengi vitongojini mwa mji kuu Lusaka, lakini sasa inaonekana yanasambaa kwengineko.

Chanda amesema maeneo ya mikusanyiko mikubwa ya watu yatakayobainika kuchochea usambazaji wa maradhi hayo kama vile baa, migahawa na hata masoko – yatabidi yafungwe kwa mda hadi hali ya usafi iimarishwe zaidi.

Ametaka vikosi hivyo vya wanajeshi kusaidia zaidi katika huduma za usafi kama njia mojawapo ya kukabiliana na mlipuko wa magonjwa hayo hatari lakini yanayoweza kuzuiliwa kwa haraka iwapo hatua muafaka zitachukuliwa.

LEAVE A REPLY