Rais Recep Erdogan atangaza hali ya hatari Uturuki

0
200

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza hali ya hatari na kutoa amri ya kutotembea usiku kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo hii ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kwa jaribio la mapinduzi ya serikali yake.

Mpaka sasa serikali ya Uturuki imeshatangaza kupiga marufuku wasomi wan chi hiyo kusafiri nje ya nchi huku zaidi ya shule 600 zikiwa zimefungwa na zaidi ya watumishi 8,000 wa serikali wakiwa wamefutwa kazi na zaidi ya wanajeshi 2,000 wakiwa wamekamatwa kwa kutuhumiwa kuhusika na uhaini.

Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na makamanda wa majeshi ya nchi hiyo wanaodaiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi pamoja na raia wanaotuhumiwa kuunga mkono jaribio hilo.

Rais Erdogan amekanusha kuwa hatua hiyo haimaanishi kunyima uhuru na haki za wananchi wan chi hiyo isipokuwa ni hatua muhimu ili kuimarisha usalama wan chi hiyo katika kipindi hiki.

‘Hatua hii haiendi kinyume na demokrasia, sheria na uhuru kwa namna yoyote ile’ amesema rais Erdogan.

Watu wanaompinga rais Erdogan wanadhani kuwa hatua hiyo inatumiwa na rais huyo kujiimarisha madarakani na kutengeneza mwanya wa kujiongezea muda wa kukaa madarakani.

Wakati huo huo rais wa Uturuki amesisitiza kuwa serikali yake ina ushahidi wa kuthibitisha kuwa mhubiri na msomi wan chi hiyo anaishi marekani Fetullah Gullen anahusika na njama za jaribio hilo la mapinduzi.

Uturuki inatarajia kutuma ushahidi huo nchini Marekani ili kuthibitisha madai hayo na kisha kuiomba Marekani imrudishe Gullen nchini Uturuki.

Mhaini?: Mhadhiri Fettulah Gullen anatuhumiwa kuhusika na jaribio la mapinduzi nchini Uturuki
Mhaini?: Mhadhiri Fettulah Gullen anatuhumiwa kuhusika na jaribio la mapinduzi nchini Uturuki

LEAVE A REPLY