Rais Mutharika aamuru kukamatwa kwa ‘fisi’ Eric Aniva

0
413

Rais wa Malawi Peter Mutharika ameamrisha kukamatwa kwa raia wake Eric Aniva aliyehojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC kuhusu ushiriki wake kwenye mila ya kuwasafisha wasichana na wajane.

Kwenye mahojiano hayo, Eric alielezea kwa undani jukumu lake la kufanya mapenzi na wanawake hao ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa kabila lao ili kuwasafisha kutokana na mabalaa yanayoweza kuwakumba.

Polisi wameshamkamata Eric na anatarajia kufunguliwa mashtaka ya kuvunja haki za watoto.

Rais Mutharika amekiri kusikitishwa na kuchukizwa na kile maelezo yaliyotolewa na Aniva kwenye mahojiano na BBC na amedhamiria kuikomesha mila hiyo.

Bw. Eric Aniva ambaye ni muathirika wa VVU ameshawahi kushiriki mapenzi na wanawake na wasichana zaidi ya 100 kwenye jamii hiyo tang mwaka 1985 ikiwa ni sehemu ya tamaduni ya kuwatakasa wasichana wanawari na wajane.

Utamaduni huo wa utakaso wa mwili kwa njia ya kufanya mapenzi na wanaume maalum waliopewa jina la ‘fisi’ hugharamiwa na familia za wanawake na imekuwa na umekuwa na hadhi kwenye jamii za kusini mwa Malawi ingawa serikali ya nchi hiyo imekuwa ikipambana kuukomesha.

LEAVE A REPLY