Rais Magufuli kuzindua tawi la CRDB Chato

0
153

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua tawi la benki ya CRDB katika jengo jipya lililopo eneo la mlimani mjini Chato mkoani Geita.

Taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa Wilaya ya Chato Shaban Ntarambe, inaeleza kuwa hafla ya uzinduzi wa tawi hilo itaanza saa mbili asubuhi katika eneo lilipo jengo jipya la benki hiyo.

Ntarambe amewataka wananchi wa Chato na maeneo ya jirani kujitokeza kumsikiliza rais na kushuhudia uzinduzi huo ambao unaendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa mjini Chato wamepongeza juhudi zinazofanywa na wadau wa maendeleo kusogeza huduma karibu na wananchi na kusema Chato ya sasa sio kama ya zamani na kwamba, uwepo wa miundombinu hiyo inafungua maendeleo.

LEAVE A REPLY