Rais Magufuli azindua kiwanda cha maji cha JWTZ

0
469

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua Kituo cha Uwekezaji cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia SUMA-JKT kilichopo eneo la Mgulani jijini Dar es Salaam.

Kituo hicho kina Kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi, Shule ya Sekondari Jitegemee na Ukumbi wa Mikutano.

Rais Magufuli amesema atakuwa mdau mkubwa wa kununua maji ya Uhuru Peak yanayotengenezwa na kiwanda hicho akizisihi pia kwa taasisi na ofisi za serikali ikiwezekana zitumie maji hayo maofisini mwao badala ya kutumia maji mengine ili kuongeza uchumi na kusapoti viwanda vya JWTZ na vya serikali kwa jumla.

“Kuanzia leo mimi nitakuwa mdau mkubwa wa kutumia maji yenu ya Uhuru Peak, nitashangaa sana kukuta CDF, kiongozi yeyote wa Jeshi la Ulinzi au mkuu wa mkoa ananikaribisha ofisini kwake halafu nakuta kuna maji mengine tofauti na ya Uhuru Peak.

 Pia Rais aliomba chupa ya maji hayo ya Uhuru Peak na kunywa papohapo, huku akiagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda naye apewe na anywe papohapo na kwamba Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi apewe, ili ayanywe wakati akifungua mfungo wa Ramadhan  jioni.

LEAVE A REPLY