Rais Magufuli awaachia huru Babu Seya na Papii Kocha

0
282

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli leo amewaachia huru mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaw Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha.

Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo katika sherehe za miaka 56 za Uhuru wa Tanzania Bra zinazofanyika mkoani Dodoma.

Rais Magufuli amesema kuwa kuanzia leo amewasamehe wanamuziki hao baada ya kukaa jela zaidi ya miaka 13.

Babu Seya na mwanawe Papii Kocha walifungwa miaka 13 iliyopita baada ya kukutwa na hatia ya kunajisi watoto na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Babu Seya alifungwa na watoto wake watu ambapo wawili walifanikiwa kutoka miaka ya njuma kutokana na kukata rufaa lakini Babu Seya na Papii Kocha rufaa yao iligoma hivyo wakatumikia jela kifungo cha maisha mpaka leo wameachiwa kwa msamaha wa Rais.

LEAVE A REPLY