Rais Magufuli aonya mapigano ya wakulima na wafugaji

0
90

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufli amewataka Wakulima na Wafugaji kuacha vitendo vya kupigana kwa kugombania ardhi.

Rais Magufuli amesema kwamba kamwe vitendo vya kupigana visirudie katika serikali yake na kwamba wale watakaokiuka watashughulikiwa.

Aliongeza kuwa anataka wakulima na wafugaji waishi kwa kuheshimiana kwani yeye anachokihitaji ni amani.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewashangaa Wafugaji kuwalisha ng’ombe mazao ya wakulima ilhali kuna majani ya kutosha na wanaposhtakiwa wanaamua kutumia gharama kubwa kuhonga hata kufikia hatua ya kuuza ng’ombe.

Pia Rais amesema kuwa kama yupo mmoja ambaye analiisha kila siku anajifanya ana mali huyo mimi ndiye ntalala naye mbele mwenyewe.

LEAVE A REPLY